FAQs

Frequently Asked Questions

Meticulous General Insurance Company Limited imeanzishwa mwaka 2006 wakati huo ikiitwa Momentum Tanzania Insurance Company Limited na ilikuwa ikishughulika na bima za afya (Medical), mwaka 2009 ikabadilisha jina na kuwa Metropolitan Tanzania Insurance Company Limited ambalo jina hili lilidumu kwa miaka 12 hadi mwezi June mwaka 2021 na kuwa METICULOUS GENERAL INSURANCE COMPANY LIMITED, tangu hapo kampuni imekuwa ikifanya vizuri kwenye ukuwaji na ugawaji wa soko pia (Growth and Market Share ya zaidi ya asilimia 92 mwaka 2021/2022)

Meticulous General Insurance Company Limited inatoa huduma za bima mbali mbali isipokuwa bima ya afya kwa sasa tumesitisha. Kampuni yetu inajikita zaidi na kutoa suluhisho kwa wateja wetu ili tu kuwaridhisha na kuwafanya warudi tena kwa ajili ya huduma zetu. Bima kama za nyumba, viwanda, fedha, vyombo vya moto (magari, pikipiki, bajaj) bima za ajali na nyingine nyingi...

Ndio, bima ya moto ni muhimu kwenye kila biashara na makazi ya watu, kwani majanga ya moto hayaepukiki na haijulikani muda gani janga hilo litatokea. Tupigie sasa tukupatie suuhisho la biashara yako kwenye majanga ya moto na wizi ili kulinda bishara na uchumi wako.